UTETEZI LAINI USIO NA MASHIKO WA DR KITILA MKUMBO


Hbari ifuatayo ni kwa hisani ya gazeti la Raia Mwema.
Ndugu wanajamvi, nimeona ni vema kujadili mada hii ya kwasababu kuu mbili.
1. Imelenga kupotosha ukweli wa mambo kuhusiana na mgogoro
2. Kwa kiasi fulani umeonekana kujibu au kujadili hoja za wana duru kwa njia ya kiufundi.

Nimezigawa hoja katika namba ili ziweze kusomeka na kuangaliwa kwa macho mawili.

UPOTOSHAJI
1. Dr Kitila hakueleza chanzo cha mgogoro. Alichokieleza ni watu kuumbuliwa kama wasaliti na wahaini wanapopingana na uongozi(point#5).

Kitila anafahamu kuwa yeye na wenzake hawakuongoza jitihada za kupinga uongozi, walichokifanya ni jitihada za kuleta mtafaruku.

Kwanza, kutumia waraka ambao kupitia mitandao ya kijamii ilikuwa inatoa hoja za waraka kwa vipengele(Rejea bandiko#92 kwa mfano).

Kitila anapingana na hoja yake#10 kwamba migogoro ya kisiasa hutatuliwa kwa mazungumzo. Kitila na wenzake hawakutumia mazungumzo,walitumia waraka.

Lakini pia anapingana na hoja yake#15 ya viongozi kuyamaliza na kuitisha uchaguzi.
Kitila hakutumia njia hizo alichokifanya ni kujificha na kuandika waraka ambao amekiri kushiriki.

2. Hoja#8, Kitila amepotosha kusema Mbeki aliondolewa na Zuma katika uchaguzi.
Ukweli ni kuwa Mbeki aliondolewa na kamati kuu ya ANC miezi 8 kabla ya uchaguzi.
Aliyekaimu nafasi hiyo ni K.Motlanthe.

Hoja ya Urais wa A.kusini ulitoka kwa Mbeki na kwenda kwa Zuma kwa njia ya kura ni upotoshaji

Hata hivyo, Kitila atambue kuwa kamati kuu ya ANC ilichukua hatua baada ya kubaini Zuma hakuwa na makosa mbele ya mahakama.

Ni uamuzi kama huo ambao kamati kuu ya CDM iliutumia katika kuwavua vyeo wahusika ingawa halikuwa suala la mhakamani. Hivyo hapa anajichanganya kwa kulaani maamuzi ya CC ya CDM na kuunga mkono maamuzi ya CC ya ANC.

3. Hoja#14, Kitila anaueleza umma kuwa sababu viongozi kuondolewa wadhifa ni za utatanishi. Hakuna utatanishi katika waraka aliokiri ameuandika na ambao ulishaanza kufanyiwa kazi.

4.Hoja#10, Kitila anasema njia ya kutatua migogoro ni kuhakikisha haisababishi madhara kwa taasisi. Ukweli kuwa waraka haikuwa njia nzuri na mgogoro uliopo ni matokeo tu.

Laiti angekuwa ana 'walk the talk' asingeandika kitu kinachosababisha mgogoro na kuzorotesha upinzani.Kitila na wenza hawakutimiza hoja# 9 inayowataka kutatua migogoro kwa kukaa pamoja.

5. Katika hoja#1 na 2, Kitila amemtaja kiongozi wa upinzani kushindwa kushughulikia suala la mawaziri na amesema hiyo ilikuwa fursa ya kuimaliza CCM kwasababu samaki huoza kuanzia kichwani. Amesahau aliyekuwa naibu kiongozi wa upinzani alianzisha tuhuma ambazo CCM wangekuwa makini tuhuma huenda zingeimaliza CDM, Kitila anahubiri kitu ambacho anafahamu kingiemaliza CDM lakini akitaka kiimalize CCM. Double standards.

Mkumbo aelewe kuwa kiongozi wa upinzani ni mtu lakini upinzani ni kundi ambalo washirika wake wamo. Ingelikuwa busara angetumia neno upinzani bila kumtaja kiongozi, tunajua ni Mbowe.

Kwa hili ameonyesha sentiment zaidi ya kujenga hoja kama alivyoonyesha katika waraka na kama alivyoonyesha katika hoja#10.

6, Hoja#14, si kweli kuwa vyama vya siasa vinajengwa na wafuasi.
Ukweli ni kuwa wafuasi wanajenga chama kwa kuamini katika sera za chama na misimamo yake.

Chama kinachojengwa na mtu ni genge la watu na si chama au taasisi.
Hoja ya kusema mbunge mwenye wafuasi akifukuzwa chama kitakufa au kutetereka ina mashiko tu kwa chama kinachoamini katika personality na si policy.
Sijui CDM ambayo yeye alikuwa mshauri kinaamini katika nini.

7. Hoja#13, Kitila anasema wanachama wanaodhani kufukuza watu wanakosa mantiki, nadhani Kitila anakosa mantiki kabla yao.
Mifano ipo hai, TANU iliwahi kugawanyika na kuundwa kwa AMNUT na UTP.
ANC imegawanyika makundi mawili, lile lililounda chama kumuunga mkono Mbeki na lile la Malema.Huko nyuma ANC iliwahi kuvunjika na kuunda PAC.
Rainbow alliance ilivunjika na kuunda ODM na Jubilee.

Mifano hiyo inaonyesha kuwa kama lipo kundi lisiloridhika na mambo na jitihada za kurekebisha zimeshindika ipo plan B ambayo ni kujitenga na kuondoka na wafuasi kwa kuanzisha chama kingine. Mrema aliawahi kufanya hivyo bila kuathiri taasisi nyingine

Nadhani hiyo suluhu ingeweza kutumiwa na akina Mkumbo na washirika wake badala ya kujificha na kuandika waraka wa uchochezi.Makundi niliyoyataja yalifanya mambo yao hadharani na si chini ya kapeti kama ilivyokuwa kwa Kitila and associates.

Nyerere, Mandela, Clinton, Blair, Washington, Gandhi n.k. walikuwepo na wameondoka na vyama vyao bado vipo.

Mrema aliondoka na wafuasi na CCM ipo, Lamwai aliondoka na wafuasi na NCCR ipo, Mapalala alindoka na wafuasi na CUF ipo n.k.

Sidhani katika siasa za kileo chama kinajengwa kwa jina. Kama ni hivyo Kitila anavyodai hakuna sababu za CDM kunadi sera, kianchotakiwa ni kunadi sura ya mtu.
Siasa za kileo hazikubaliani na hilo.

MAONI
Ukisoma makala ya Dr Kitila ni dhahiri bado anaamini kuwa alichotaka kukifanya kwa kuandika waraka kilikuwa sahihi.

Kitila anaweza kuamini hivyo na wala si kosa, lakini kiongozi kama yeye anapojitokeza na kuomba radhi halafu kurudi magazetini kuandika kile kile alichokiombea radhi inatia shaka na kusikitisha.

Kitila na wenzake hawakutumia njia za kidemokrasia katika kupingana ndani ya chama chao. Walichokifanya ilikuwa ni uchochezi kwa kutumia mitandao ya jamii.
Hili ndilo kitila analosema ni demokrasia na lazima vyama vivumilie.

Zuma hakuandika waraka wa siri alipambana kwa uwazi.
Kitila na timu yake hawana historia ya kujitokeza na kupambana wazi katika misingi ya demokrasia, leo anapata wapi ushujaa wa kuhubiri demokrasia ambayo hakuwahi kuifanya?

Kitila anasema ni vema mgogoro ukamilizwa kwa njia ya uchaguzi.
Hilo ndilo alipaswa kusema hata kabla ya kuandika waraka.

Alichokifanya ni kaundika waraka ili kuchochea uchaguzi na si kudai uchaguzi.
Ni makosa kudhani kuwa demokrasia inaruhusu uchochezi na si taratibu, hiyo si demokrasia ni vurugu.

Endapo anadhani wanachama wana haki ya kumaliza mgogoro kwa uchaguzi, Kitila ana halalisha maasi ndani ya chama kama sehemu ya demokrasia.

Leo Zitto anaweza kuwa kiongozi wa CDM, anachosema Kitila ni kuwa atokee mwanachama na kuleta vurugu ili suluhu iwe uchaguzi.

Chama hicho sijui ni cha kisiasa au ni Simba na Yanga.
Sidhani CDM wamefika huko na kama huo ndio ushauri basi lipo tatizo kubwa zaidi.

Tena anasisitiza kuwa kuandika waraka na kutuma katika mitandao ili uchaguzi ufanyike ni njia ya kiistaarabu ya kumaliza mgogoro.

Dr amesahau kuwa waraka haukuwa njia ya kistaarabu na ndio chanzo cha kufumua timbwili la sasa na kwamba vurugu zilianza siku nyingi tangu alipomtetea Juliana kwa hoja 'aachwe abalehe'.

Hivi vurugu zinakuwaje sehemu ya demokrasia? Mimi nilidhani demokrasia ndio sehemu ya suluhisho  la vurugu, inaonekana bado nahhitaji kusoma maana ya demokrasia zaidi, nitafanya hivyo na namshukuru Dr Kitila kwa kunisukuma nirudi maktaba.

Hadi hapo nitakapokubaliana naye, kwasasa nabaki kusema kuwa anachokifanya ni kuendeleza mgogoro, kumtetea mshirika wake asifukuzwe.

Kufukuzwa au kutofukuzwa hilo ni suala la wanachama wa CDM lakini muhimu ni Kitila kutambua kuwa CDM ijengwe kama taasisi na si mtu.

Mandela alisema watu na viongozi wapo na wanapita, taasisi ipo siku zote.
Hii dhana ya kuwa fulani amefanya kazi sana na anawafuasi ni dhana hafifu.
Umaarufu utumike kujenga chama na si kubomoa chama.

Kwa andiko la Kitila nadhani anchochea kuni badala ya kutia maji.

No comments:

Post a Comment