Chupi huwa tunaidharau lakini ina mdomo mkali
Chupi chafu na inayotoa kharufu mvaaji naye ni mchafu
Chupi yenye mikato ya kike nayo huongea kwa kike-kike
Chupi hiyo huitwa "brief" na mvaaji ana taswira ya kike
Pengine hujui lakini chupi humsema mwanaumme pia!
Chupi kama kaptura hii yaitwa "Boxer" for real men.
Chupi hiyo huficha mapaja kuashiria si lolote lile.
Chupi ya "Brief" hutukuza mapaja na haimfai dume.
Chupi ya "Boxer" kauli yake ni kuwa mvaaji ni kidume.
Pengine hujui lakini chupi humsema mwanaumme pia!
Kama chupi havai basi naye huyo ni kioja kitupu!
Kama chupi havai suruali kwake ndiyo chupi yake!
Kama chupi havai suruali yake sasa ndiyo jamvi!
Kama chupi havai suruali yake sasa ndiyo taulo!
Pengine hujui lakini chupi humsema mwanaumme pia!
"Boxer" ni funga kazi na mwanaumme apaswa kujivunia.
"Boxer" imeshinda hata wadada waionapo wamkubali mvaaji.
"Boxer" hujivunia mwandani wa mvaaji na hata kumzawadia.
"Boxer" ni ghali dukani lakini jipinde uinunue na kuimiliki.
Pengine hujui lakini chupi humsema mwanaumme mvaaji pia!
No comments:
Post a Comment