Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa pingamizi lililowekwa na Zitto Kabwe mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu ya chadema kesho limetupiliwa mbali.
pingamizi hilo ambalo lilikuwa ya kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu. Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake
Wanasheria wa CHADEMA walifanikiwa kupangua pingamizi hilo wakiongozwa na Tundu Lissu pingamizi hilo ambalo lilienda kwa hati ya dharura. huku upande wa Zitto ukiwakilishwa na wakili wa hati za viwanja Alberto Msando.
Ajenda za kesho zilizo mtisha Zitto ni hizi
Mkutano Maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;
Mosi; Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba
Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria
ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa
2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya
Katiba Mpya.
Pili; Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.
Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha
utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa
ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya
kikao kinachohusika.
Tatu; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014
Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati
wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati
makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.
No comments:
Post a Comment