Watanzania Kwanini Tusiongee Ukweli wetu tuujuao..Nchi ni yetu tusipoongea sisi nani atatuongelea..
Daktari wetu wa Watanzania anaomba aongezewe mshahara lau ufike
Tshs3,500,000(2,200USD) kwa Mwezi..anaambulia jibu l a “SINA PESA” Kwa
Nchi hii yenye Neema kulikoni Zote Duniani, Hii si aibu kubwa kwetu sisi
wenye nchi.. U
kienda Mbele zaidi unaweza kuhoji kwani hapo awali viumbe hawa,walikuwa
wanalipwa Kiasi gani , kuna mtu atakwambia ni kiasi Fulani Chini ya
Milioni Moja, kama 860,000 na Take Home yake 720,000(461USD) haya Ni
maafa kwa Daktari wa Binadamu mwenzie. Kuna Jambo Limetufanya wengine
tugande siku mbili hizi pale tuliposikia kwamba mkuu wa Kaya Hili la
Watanzania ametamka waziwazi kwamba kiasi hicho ni kikubwa na hakiwezi
Kulipika.. Inatisha sana sentensi hii ..”SINA HELA”
Mbali na Hapo nikaona wenzetu wengi wameweka takwimu za mishahara ya
madaktari kwenye kanda ya Nchi mbalimbali Afrika humu jamvini.. na
kwamba TZ ikaonekana ndio inayowalipa watanzania wake hawa vijisent
kiduuchu, mimi si mtaalam wa takwim hizi ila niliwapigia cm marafiki
zetu wa Libya hata na wewe unaweza kuwapigia +353 85 134 3515 , Mshahara
wa RMO umefikia zaidi ya 8million za kitanzania, mbali na Nyumba na
Food allowances, matibabu na security na anafanya kazi wiki tatu za
mwezi. T
anzania si NCHI ya KUFANANISHAna nchi yoyote barani Afrika na Duniani
kwa ujumla, ni nchi ya kipekee inayojibeba kwa kusheheni Utajiri
uliopitiliza.
Tanzania ina zaidi ya Mito 46, Mto Ambala , Bangala , Great Ruaha, Kafufu, Kagera, Kalambo, Kilasi, Kipoke, Kiwira , Luhumuka, Lukuledi, Lumi, Magamba , Malagarasi , Manonga , Mara, Marogala,Mbaka ,Mkulumuzi ,Mkuzu ,Mrambo,Msangazi,Mulagala,Mwatisi,Myakaliza ,Ngerengere ,Pangani ,Rufiji ,Rurubu , Ruvuma , Ruvyironza,Selian,Semu ,Sibiti ,Sinini,Suma ,Ulanga,Ulanga ,Umba River, Wami ,Wembere,Zigi
Mito hii ina mamilioni ya samaki wanozaliana kila mchao, Ila wewe
“SINA HELA” Tanzania yako bado wananchi wanakula takataka, wanavimbiana
kiunoni hadi .., mito yenye maporomoko na uoto wa ajabu.
Tanzania ina Maziwa Mengi Makubwa ya Kimataifa, Ziwa Ambussel, Babati, Burigi, Chala, Eyasi, Ikimba, Jipe, Kitangiri, Manyara, Mdutu, Natron, Nyumba ya Mungu Reservoir, Rukwa, Sagara, Tanganyika, Victoria .. Achilia Mbali Mbuga za Wanyama Kubwa sana lakini zimechukua asilimia 4.4 ya eneo la nchi yetu, Mbuga
za Arusha, Gombe Stream, Jozani Chawaka, Katavi, Kilimanjaro, Kitulo,
Lake manyara, Mahale,Mikumi, Maunt Meru, Ruaha, Rubondo, Saadani,
Serengeti, Tarangire, Udzungwa
Umewahi kusikia Hifadhi za Kisiwa Cha Mafia, chenye nchi chini ndani ya
maji, bahari mavu, ukizama chini ya bahari yake unakuta majani mengi tu
(sea grass) tena maji yake masafi utadhani ni mbuga za wanyama chini ya
Bahari, Umewahi kusikia Mnazi Bay kijieneo kidogo ha bahari kama
Kilometa za mraba 650, lakini kimesheheni samaki aina 440, nadhani
mwenzangu umeshasikia juu ya Ngorongoro Kreta, sehemu ya mchoto mkubwa
wa meguko la kivolkeno la mlima mkubwa ulioacha uwanda mkubwa usio na
maji AMBAO hakuna kama hivi Duniani.. ni maajabu makubwa sana ndani ya
Tz inayosema “SINA HELA”, wanasema nyayo za mwanadamu wa kale
ziligunduliwa hapo, mwanamke Daktari leakey akagundua Fuvu la mwanadamu
wa kale zaidi. Mie najaribika kusema Edeni labda ilikuwa Tanzania..
Utajiri wote huu.. “SINA HELA”.. mie sijui kama weye umeshasikia habari
za Ndege wanaotengeneza michoro angani, ndege wanaoruka kama waoteao
shambulizi hapo naongelea hifadhi ya Selous. Niseme nini “SINA HELA
UNIELEWE??”
Tanzania yenye madini ya kila aina, Nikuulize ‘SINA HELA” embu Tafuta
ni madini gani hapa Duniani hayapo TANZANIA, Kila Madini kila kito TZ ni
asili yake, Zaidi ya Yote Mwenyezi Mungu ameweka upendeleo maalum na
kutulazia Madini ambayo ni yetu tu, hayapo pengine kwenye dunia Yote,
TANZANITE, nani anabisha.. “SINA HELA”.
Mbali na Uranium, Leo hii Tuna Mafuta, Vitalu nane vyenye ratili za
mafuta laini yenye thamani sana Duniani. Nikikupa ujazo wa gesi
tuliyonayo Tanzania ikiuzwa kwa usahihi kwa soko la ndani linatosha
kuibeba bajeti kwa asilimia 89. Tukisema hivi mtu atasema tunakuza
jambo, lipi tumekuza mbumbumbu wa kufikiri wewe. Mvivu wa kutumia
kichwa, unatia joto kiti cha ofisi kwa kutengeneza midokezo ya posho
kila siku na kuvizia visafari vya kukabana, bingwa wa kukopi vibajeti
mwaka hadi mwaka unazidisha kwa 5%icrement.. Mvivu hadi nywele zako
zinakusuta.. fia mbali kulee..
‘SINA HELA” karne hii nchini kwako bado wananchi wako wanalima kwa jembe
la mkono, miaka hamsini ya Uhuru, tukisema mawazo yamerogwa na
yakarogeka ni uongo? Leo Daktari maskini ya Mungu anaomba kamshahara
kiduchu unamaka “SINA HELA” kama unaona haitoshi “TIMUA” UNAFUNGA
MJADALA, UNAONDOKA , full stop, aisee, aisee!! .. Uvivu wa viongozi wetu
kufikiri ndio unaoburuza taifa..
Taifa ni Letu kwanini TUSISEMEE.. tusiposema sisi machozi ya watoto wetu
yatatusuta..kila mtu ni mzazi ana familia, kila mtu ana haki ya kusema,
kama hutaki mtu aseme UA..
Kiongozi bora hupima kila changamoto na kuijaribu lakini si kuikataa na
kuipinga kwa kunyofoa watu wake kucha na meno bila ganzi.. aisee
IMENIUMA SANA..
Sijamaliza kuchimbua utajiri wa nchi hii isiyo na ukabila, isiyo na
Udini, isiyo na Lugha changanyiko, kila mtu anajua Swahili, Nchi
Tulivu.. , sijaenda kwenye mazao.. ‘SINA HELA” basi hiyo slogan
“SINA HELA” ingekuwa na uwiano, Unaposema SINA hela basi hata nyumbani
kwako uwe kweli huna hela watu watasema huyu bwana muungwana. Sasa
unaposema sina hela huku watoto wako (mawaziri) wakijenga Dream Houses
ufukweni, wanabadili magari ya kifahari kama mashati, wanatenda
wanavyotaka halafu unasema”SINA HELA” Huu ni Ungwana?,
Kuna Shule siku hizi zinaitwa English Medium, ada yake ni nene sana
kiasi, kuna nyingine hadi milioni 14 kwa mwaka kama ada ya mototo. Na
wanaosoma huko ni watanzania watoto wa watanzania.. sasa hii Fortune
ndani ya nchi hii hawa wenzetu wameitoa wapi kama “SINA HELA” ina uwiano
sawia? Huku mnatujengea shule sizizo na walimu na ambazo wanafunzi
wanasogeza umri tu na kupotezea muda. Watoto wa “HAO” wala hawasomi
shule za kata. Ni zetu mliotubagua..
Tusiseme, tukisema mnaandaa operesheni ya kunyofoa Kucha na meno bila
ganzi, na kuponda maeneo Mwenyezi Mungu aliyoamuru yalete Uzao?
Tanzania yetu ni nchi ya Kipekee, hakuna nchi ya kuifananisha Duniani,
Ina ziwa lenye kina Kirefu kuliko yote Duniani,-Tanganyika, Ina mlima wa
Pili kuliko yote Duniani na wa kwanza mrefu Barani, wanasema Africa
Watch. Huwezi kuifananisha Tanzania na japan au Korea ambapo hakuna
Madini hata tone wala Mbuga za wanyama..
Mimi nasema Madaktari wangedai Mshahara kuanzia Milioni 15 kwa mwezi
kwa kuanzia, Nchi kama Japan ambayo haina Madini hata tone, Haina ardhi
ya kutosha by then ardhi yenyewe miambamiamba tu, haina mbuga za
wanyama.. daktari wake anaanza na Mshahara wa Japan Yen 1,000,000 sawa
na Milioni 19.7za Kitanzania(1YEN = 19.7 Tshs), sasa Daktari wetu
akisema anaanzia mil 15 kosa lake nini, kwenye nchi Tajiri kama hii.
Fikirini Mtapata vipi fedha ndio maana ya Uongozi sio kunyofua Kucha
watu. Shame!!. Utasema inshu za Uchumi, Utakuwa Mshamba wa karne weye,
Japan wasiojua Lugha nyingine, japan inayozungukwa na maadui, japan nchi
ya watu wanye aibu, WANACHOKIFANYA KIPI SISI HATUKIWEZI?.. kama ni
Hummer Technolpgy sisi nani katuzuia.. Kulalama kulalama.. SIWEZI..
SIWEZI.. MI SIWEZI.. Mbona bingwa wa kuzaa na kuzalisha.. shit…
Mimi siwezi wala sithubutu kuongelea mishahara wa kada Nyingine, Eti
wahandisi, Kwani Tanzania Kuna wahandisi, au ni Ubatizo waliotupa ERB na
sisi tunajiita Eng, Kufukuzia vitenda vya kuziba barabara viraka
ambavyo unahonga mpaka unachakaa kabla ya kukipata, utamwita mhandisi
huyo, barabara ya mbagala juzi tu imetengenezwa lakini wahandisi
tumeshindwa kusimamia ijengwe kwa viwango leo imekuwa kama chapati..
Rushwa na Ujinga, FTC anaitwa Mhandisi wa Wilaya, huyo huyo anaingia
kwenye vikao vinavojadili barabara, maji, umeme, ukichunguza cheti ana
FTC ya welding.. Fani ya Uhandisi Tanzania Tumejidhalilisha,
Tumedhalilishwa, na nadhani Tumeridhika Kudhalilishwa.. INATOSHA!!
Unamlipa Mhandisi Tsh420,000 Gross na Net 360,000, kwa mwezi, Kisha
mhandisi huyo utamkuta ana gari, kila siku mafuta ya 20,000 (sawa na
600,000) kwa mwezi kwenda kazini na kurudi, anapata wapi hela hizi na
yeye mshahara wake ni nusu ya gharama za mafuta.. Mwizi HUYU.. MWIZIII!!
Hata kama Ukichuki Mwizi tu.. System Imekulazimisha uwe Mwizi.. na wewe
umeikubali.. Mdhambi tu..
Wabunge wetu ndio Usiseme, Kijiposho tunachowapigia kelele chenyewe
kiduuchu, sasa Wako Hoi bin dhoofu, Walipoona mshahara wakakurupukia
mikopo, sasa inawatafuna, wengine sasa hata pa kukaa gharama kubwa
Dodoma, wanalala kwenye nyumba za Ibaada na kwenye vihoteli vya
uchochoroni Hali ni mbaya kila mtu isipokuwa wajanja wachache ambao
ukiwazungumzia wanakungoa meno na kucha bila ganzi.. Mbona mtatung’oa
wengi .. kwa maisha mliyotupa bora mtusaidie tu kutuwahisha kwa muumba
tuwaachie Dunia yenu wajinga wakubwa..
Mimi Bihagaze nadhani kuna haja ya fani zote za ualimu, uhandisi,
uchumi, kuamka kama wanavyoamka madaktari, kuiwajibisha serikali
ifikiri na kufanya kazi ya kutumia rasilimali za nchi hii kwa ajili ya
wananchi wenyewe, Huo ndio Uongozi sio kutia Joto Viti vya wachina na
“Eliza”, Kama Huwezi HUJALAZIMISHWA.. Ulizia Migodi, ulizia
viwanda, ulizia hata baaadhi ya Mbuga za wanyama 100% zinamilikiwa na
wageni, wewe Tanzania unaaambulia nini? “SINA HELA” Kama
mliokasmiwa madaraka hamuwezi muondoke na safu nyingine iingie kufanya
kile wanachodhani wanataka kufanya kwa maslahi ya Nchi yao.
HII NI NCHI YETU SOTE SIO YA KIKUNDI FuLANi PEKEE.. TUSITISHANE..
No comments:
Post a Comment