JAMIIFORUMS ni mshauri wa Zitto Kabwe?

Jana na leo kulikuwa na mnyukano ndani ya JF kukiwa na kuhusishwa mmiliki wa JF kuwa anatoa siri za members(wanachama) na leo asubuhi nikaona timbwili linaendelea lakini kila linapoibuka anayelianzisha lazima kifungo kimhusu...
mfano ni huyu

katika gazeti la mawio la jana alhamisi tarehe 26/12/2013 kulikuwa na taarifa nzito juu ya
mwandani wa zitto kutoa siri hadharani....
Miongoni mwa watu waliotajwa katika gazeti hilokuwa wanaukaribu mkubwa na zitto ni wewe
ndugu mkurugenzi wa mtandao huu azimu waJF.....
sitaki kuingilia haki yako binafsi ya kuwa na uhusiano na watu laa bali nimejenga shaka
pengine na members wenzangu wa JF juu yauhusiano wako na ndugu zitto unaohusishwa na
harakati zinazoendelea chadema je samahani lakini una lolote la kuueleza umma ukweli juu ya
kile kilichoripotiwa?? ufafanuzi wako utaondoa ukakasi juu ya hofu ya mgongano wa kimaslahi
baina yako kwa upande mmoja na kwetu wanaukumbi ambao ni watu wa vyama tofauti..
Nimeandika hili kutokana na heshima uliyonayokatika jamii hivyo ni bora ukatueleza uhalisia wa
kilichoripotiwa na gazeti la mawio.
jambo la pili ni je kuna ukweli kwamba bi. josephine mushumbusi alipiga simu hapo jf
kuulizia habari za uzi uliofutika ambao ulipostiwa na Yericko Nyerere? na je unatuhakikishia vipi
kwamba hakuna hujuma au upendeleo wenyemrengo wa kimakundi na kivyama ndani ya JF?
mwisho kabisa nakutakia msimu mwema wa sikukuu nikitumaini utatoa maelezo ya kina juu ya
kile kilichoripotiwa na MAWIO,,,natanguliza shukrani na samahani kwa kukuandikia barua ndefu kama hii.

Majibu ya Maxence Melo Mubyanzi akilijibu mawio la tarehe 25/12/2015
Nimearifiwa na Moderators kuwa kuna habari imenitaja na nikaombwa niitolee ufafanuzi mapema.Niseme ninasikitishwa sana na aina ya uandishi  inayoendelea nchini na pia niseme udhaifu wa serikali yetu (japo hawataki isemwe hivyo) ndio uliotufikisha hapa.Siwezi kusema nitawaburuza mahakamani
Mawio kwa upotoshaji, ni kumpigia mbuzi gitaa maana ndipo tulipofikia kama taifa.

UFAFANUZI WANGU:1. Kuhusu habari ya Gazeti la Kubenea - MawioKwanza: Mimi si Mkurugenzi wa JamiiForums. JamiiForums haina Mkurugenzi hata mmoja, gazeti makini lilitakiwa kujihakikishia pasipo na
shaka kuhusu hili walau.
Pili: Nilipigiwa na Said Kubenea (wa Mawio) akaniuliza hivi: "Nina taarifa toka kwa watu wangu kuwa wewe ulimwambia Zitto kuwa mimi ndiye niliweka JF tuhuma dhidi yake".Nikiri kuwa, nilicheka kwanza kisha nikaona bora nimsikilize amalize. Alipomaliza, nikamwuliza "Uliamini hizo taarifa?" akajibu "Niliamini kiasi na ndiyo maana nikakuuliza ili nipate taarifa ya upande wako".Nilimjibu kwa kumwambia hivi "Kaka, unanifahamu, na umefanya vema kuniuliza; unadhani mimi nimwambie
Zitto kuwa aliyeleta taarifa za Zitto JF ni Kubenea ili inisaidie nini? Na kwanini nikusingizie wewe wakati tuhuma zile zililetwa na mtu anaitwa Yericko Nyerere ambaye ni verified member katika JF?"Akaniuliza: "Kwahiyo taarifa hizi si sahihi?" Nikamjibu kuwa labda ni sahihi, lakini sisi tunajua aliyeleta tuhuma hizo kwa jina halisi na hatuna sababu ya kuzungusha wala kudanganyana na mtu yeyote akiwemo yeye Zitto!Inasikitisha kuwa mwisho wa siku habari iliyoandikwa imekaa hivi. Imagine hapo ndipo
Kubenea alipokatia simu, ghafla naitwa MSHAURI WA ZITTO!

No comments:

Post a Comment