MWENYEKITI: Namwita
Mheshimiwa Tundu Lissu na badala ya Mheshimiwa Mnyaa,
Mheshimiwa
Amina Amour na Mheshimiwa Kafulila na Murtaza Magungu wajiandae.
MHE.
TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kunipatia nafasi hii
kujadili
hoja hii ya bajeti.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, hiki ni kipindi kingine tena ambacho wengine wanakiita silly
season.
Silly season, muda wa mambo ya kipuuzi, silly season.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, kila mwaka, tunakutana katika Bunge hili kuzungumza na
kupitisha
mambo ambayo tunajua hayatekelezeki. Serikali inakuja na bajeti, inakuja na
ahadi
ambapo
yenyewe inajua hazitekelezeki. (Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, Wabunge wanasimama, wanasema wanaunga mkono mia kwa
mia,
kinachofuata ni kuponda hicho walichokiunga mkono mia kwa mia kwa sababu
wanajua
deep
down ni uwongo, hakitekelezeki. (Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, kwa hiyo, this is another silly season. This is another season to
lie to
ourselves,
to lie to our children, to lie to our country. We should be ashamed of
ourselves. (Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, mwaka jana tulikuja tena kwenye silly season ya mwaka jana,
tukaambiwa
na Serikali inayojua kwamba haya mambo hayatekelezeki, tukaletewa Mpango wa
Maendeleo
wa Taifa wa miaka mitano. Serikali inayojua kwamba haya mambo hayatekelezeki,
ikatuambia
kwamba kwa maneno yao, kwa maneno ya Mpango wenyewe, kuanzia sasa
tutatenga
shilingi trilioni 8.6 ya mapato ya ndani kwa ajili ya Bajeti ya Maendeleo.
Asilimia 35
Mpango
wa Maendeleo wa miaka mitano, trilioni 43 approximately, tukaambiwa kwamba
tutatenga
kila mwaka shilingi trilioni 8.6 ili kutekeleza mpango huu, another silly
season. Tukaitwa St.
Gasper
na Mheshimiwa Rais, tukalishwa, tukanyweshwa, tukapiga makofi, mwaka huohuo
mwaka
jana,
badala ya kutenga shilingi trilioni 8.6, wakatenga trilioni 4.9, silly season.
(Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, tukahoji hapa, tukahoji kwamba mbona mmesema mtatenga
shilingi
trilioni 8.6, mbona mmetenga shilingi trilioni 4.9? Wakasema huu ni mwaka wa
mpito. Sasa
leo,
tunakutana hapa kujadiliana juu ya Mpango wa Maendelo na bajeti ambayo imetenga
shilingi
trilioni 4.5 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo, tuliambiwa, tutatenga kila mwaka
shilingi trilioni
8.6,
they knew they were lying, we knew they were lying; we should be ashamed of
ourselves.
(Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, we should be ashamed of this Government, we should be
ashamed
of this party, and we should be ashamed of these Members of Parliament
wanaopitisha
this
kind of silly thing. (Makofi)
KUHUSU
UTARATIBU
WAZIRI
WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa
Mwenyekiti!
MWENYEKITI:
Mheshimiwa Lissu naomba ukae. Mheshimiwa Lukuvi?
WAZIRI
WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa
Mwenyekiti,
kuhusu utaratibu tu, namkumbusha uncle wangu, lugha hizi za kuudhi haziruhusiwi
humu
Bungeni, tafadhali sana. Naomba tu aendelee na mchango wake, lakini lugha za
kuudhi,
Kanuni
zetu zinakataza, Kanuni ya 64.
MWENYEKITI:
Mheshimiwa Lissu, ninaamini una hoja nyingi nzuri, unaweza kuwasilisha vizuri
na
kila mmoja akaelewa, Kanuni ya 64 inatufunga kutumia maneno ya kuudhi wengine,
naomba
uchangie
hoja zako kwa uzuri, Serikali inakusikia, naomba uendelee.
MHE.
TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika Mpango wa mwaka
jana
tuliambiwa kwamba, Serikali itaziba mianya ya ukwepaji kodi, itapunguza
misamaha ya kodi.
Hii
lugha ni ya miaka mingi sana. Leo hii, mwezi huu, viongozi wetu wa kidini wa
Baraza la
Maaskofu
Tanzania wa Christian Council of Tanzania na wa BAKWATA, wametoa ripoti
wanaiita
The
One Billion Dolar Question; jinsi ambavyo Tanzania inapoteza fedha kutokana na
mianya,
ukwepaji
na misamaha ya kodi ambayo imepitishwa na Bunge hili na kila mwaka tunaambiwa
itashughulikiwa,
lakini Serikali haifanyi hivyo, Wabunge wa Chama kinachotawala hawafanyi hivyo
na
wao ndio wenye responsibility kwa sababu, wao ndio wengi. Kwa hiyo, this One
Billion Dollar
Question,
this One Billion Dollar Disaster ni disaster ya CCM and nobody else. (Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, sasa kwa wasiofahamu historia ya mambo haya, mwaka 1998,
Mheshimiwa
Dkt. Abdallah Kigoda, alikuwa Waziri wa Madini, ndiye aliyeleta Muswada wa Sheria
ya
Madini hapa. Mimi sikuwepo hapa, Mzee Cheyo, alikuwepo na kwenye Muswada,
kwenye
mjadala
wa kupitisha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998, Hansard za wakati huo, Mheshimiwa
Dkt.
Abdallah
Kigoda na Mawaziri wenzake wakati huo waliliambia Bunge hili kwamba, sekta ya
madini
italiingizia Taifa hili 52% ya revenue yote inayotokana na madini; we were
told,
walituambia,
walituahidi, leo hii viongozi wetu wa kidini wanatuambia katika mabilioni
yanayotokana
na madini yetu, tunapata an average dola milioni 100 kama kodi na mirahaba na
vitu
vinginevyo na wanasema kitu kingine kwamba, 65% ya hizo dola milioni 100
zinatokana na
kodi
za wafanyakazi. Shame on this Government, shame on this party, shame on this
people.
(Makofi)
MWENYEKITI:
Samahani. Waheshimiwa ambao mnashabikia kwa kuongea, Kanuni
zinatuzuia.
Huruhusiwi kuongea, isipokuwa kwa idhini ya Mwenyekiti au Spika. Muacheni
achangie
vizuri,
mtamshangilia huko nje.
Mheshimiwa
Tundu Lissu, tafadhali!
MHE.
TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumekuwa na dini mpya Bunge hili
na
kwa Serikali hii, tuna Miungu wapya na hawa Miungu wanaitwa wawekezaji. They
are our new
Gods,
they are untouchable; kila kitu ukifanya, eeh, wawekezaji, eeh, wawekezaji,
don’t touch
them.
Hawa ndio Miungu wetu wapya, what have they done for us out of other? No!
Madini
wanatuambia,
ni product inayoingiza more foreign exchange than any other. Hizo fedha
mlizotuambia
zitakuja ziko wapi,? We have struck up and immerse riches off our cost. Natural
gas,
kwa
utaratibu wa hawahawa, wa chama hikihiki, wa Serikali hiihii, natural gas
ambayo
imegunduliwa
off our cost itakwenda njia ileile ya dhahabu na tanzanite. (Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, sasa mimi I have lost faith completely na Serikali hii. I have lost
faith
na chama hiki. I have lost faith na watu hawa. Nawaomba Watanzania, watuunge
mkono
katika
hili. There is obsolutely no future kama nchi yetu itaendelea kuwa chini ya
watu wenye
rekodi
ya aina hii. (Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, ninaomba nimalizie maana wengine wanataka kuzungumza.
Mwalimu
Nyerere kwenye kitabu chake cha ‘Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania’, alisema
na
wala
hatuwajibiki kuendelea na chama na Serikali hii na kama tukiendeleanayo, mbele
ni giza
tupu,
majuto ni mjukuu. Watanzania wenzangu hatuhitaji kuendelea na chama hiki,
hatuendelei,
hatuhitaji
kuendelea na this kind of silly na vitu ambavyo ni vya uongo, havitekelezeki.
(Makofi)
Mheshimiwa
Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
MBUNGE
FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii sio kampeni.
No comments:
Post a Comment