ROSTAM AZIZ NA BIASHARA BINAFSI

ROSTAM AZIZ NA BIASHARA BINAFSI
KATI YA IKULU ZA TEHRAN NA MAGOGONI KUTUINGIZA MAJARIBUNI KAMA TAIFA
KATIKA USO WA JUMUIA YA KIMATAIFA

... wengine tumeonya sana tu juu ya Biashara
za Rostam Aziz kutuingiza motoni lakini hata siku moja hatukusikilizwa
na badla yake hili li-mdudu lilipewa heko kwenye jukwaa la siasa kule
Igunga na kupachikwa jina la 'Simba wa Vita'.

Yeyote anayesema kwamba kwanini tuchaguliwe marafiki;

1. kwanza tangulia kujibu swali kwamba ni lini Bunge letu tukufu kule  Dodomaliliporidhia hili zoezi la Meli za Irani kupachikwa Bendera yetu ya taifa na kuchanja mbuga kwa jina letu lakini kwa faida yao?

2. Je, maridhiano kama hayo yako kwenye Hansard ya bunge letu ukurasa wa ngapi?

3. Je, kitendo cha taifa letu kuingizwa kwenye biashara HARAMU na  HATARISHI kama hii mbele ya uso wa Jumuia ya Kimataifa, hadi leo hii taifa letu limenufaika kiasi gani cha fedha kwa kuamua kujitwisha 'kiroba cha bangi' kilichomshinda M-Irani?

4. Je, kati ya wabunge wetu zaidi ya 350 kule Dodoma, ni wangapi wanaojua undani wa makubaliano kati ya Rais Kikwete na uongozi wa Tehran?

5. Je, Iran imekua ikiifadhili CCM kupitia 'Mwekahazina wa Taifa Rostam Aziz' kwa miaka hiyo yote huku wao wakipata maslahi-rejea gani over the counter?

6. Je, iweje Zanzibar iruhusiwe kutumia jina la 'Tanzania' ambalo wako bize kila leo KULIKANA na kutaka Muungano ufe kwa haraka sana huku wakiendelea kufanyia biashara hatarishi kama hili kwa kutumia jina hilo hilo BAYA AMBALO WAKO RADHI WAFE KULIKO KUBAKIA NDANI YAKE kujinufaisha CCM kimtindo kwa ajili ya kukusanya fedha kupitia MCHONGO BINAFSI YA KUNDI MOJAWAPO NDANI YA CCM na Iran kuja kununulia tena madaraka 2015?

7. Viongozi wa CCM wanapoingiza taifa letu kwenye biashara za kunufaisha kile kinachosadikiwa kuwa ni 'ugaidi na juhudi za kigaidi kwa mapana  na marefu yake katika ukanda wetu huu na kuchinja ovyo wananchi gizani kupitia vikundi hatari vinavyofadhiliwa na serikali hiyo hiyo ya CCM' je tutawezaje kujitenga na dhambi hii kama sisi kama walazwahoi wa taifa hili hatuoni sababu yoyote ya kumwambia Dr Kikwete kwamba huko unakotupeleka HATUKO TAYARI?

NB: Swala la uhusiano binafsi kati ya Magogoni na Irani kamwe si salama kwa taifa letu kwa kuwa wananchi hata siku moja hatujawahi KUSHIRIKISHWA wala kuwekwa bayana faida na hasara zake zaidi ya kila kitu kuzungukwa na USIRI NA UFISADI WA KIFAMILIA kwa mgongo wa taifa zima. Hili halikubaliki hata kidogo hapa nyumbani na hata huko Ughaibuni.

Mwisho; sote tusisahau kukumbuka hili neno hapa - Dr Stephen Ulimboka kwa bahati mbaya sana itokee kwamba ataaga dunia au mwanaharakati mwingine yeyote yule kuguswa tena visivyo basi Magogoni wakae wakijua kwamba gharika la damu ya hao wote watakaodhurika leo ama kesho ndio itakayogeuka Tsunami la kulifunika kabisa CCM kabisa hata kabla ya jua la muula wake wa utawala wa kichakachuaji huu kuzama.

Wananchi sote tuamke na tuseme usiri katika biashara binafsi na Iran pale Ikulu lazima ikome mara moja.

No comments:

Post a Comment