Yanayozungumzwa Ministry of Foreign and
International Affairs (MFAIC) na mitaani kuhusu FITNA zilizofanywa dhidi
ya Professor Mahalu na kesi anayokabiliwa nayo mahakamani Tanzania.
1: Kwamba Balozi Mahalu alikataa begi lile la “diplomatic bag”
lisitumike katika ubebaji wa PESA toka nchi za Ulaya Mashariki
zilizopelekwa Ubalozini Roma ili zisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa
ajili ya kampeni ya URAIS ya mwaka 2005.
Inasemekana kwamba Balozi Mahalu alikataa utumiaji huo wa diplomatic bag kwani haukuwa sahihi. Kwa kuzingatia utaratibu na kanuni yeye alikomolewa kwa kufukuzwa kazi
2: Kwamba Balozi Mahalu alikataa kushiriki katika njama za kuiba pesa ya
Watanzania Euro billioni 2.4 kwani katika tathmini iliyofanywa na
Wizara ya Ujenzi kuhusu Jengo la Ubalozi, bei ya Jengo hilo lingegharimu
Euro billioni 5.5 na siyo Euro billioni 3.1 bei ambayo ndio bei ya
Jengo iliyokubaliwa chini ya usimamizi wa Balozi katika mchakato wa
ununuzi.
Wapo maofisa wa Wizara ya Nje walioshinikiza serikali inunue jingo lile
kwa Euro billioni 5.5 kwa kushirikiana na aliyekuwa Honorary Consul,
Tanzania Consulate ya Milano, marehemu Avvocato Georgio. Uadui na chuki
dhidi ya Balozi Mahalu ulitokana na hilo pia.
3: Kitendo chake cha kuwakirimu Ubalozini Maaskofu wa Kanisa la Katoliki
waliotembelea Italia kilionekana kama kurasimisha UKRISTO wa Ubalozi
pale Roma. Tuhuma hizi zipo sambamba na kile alichozusha Shehe na
Mnajimu mmoja kwamba Balozi Mahalu ni adui wa Uislamu kwani Balozi
Mahalu ndiye aliyetayarisha Memorandum of Understanding (MOU) kati ya
Serikali na Kanisa ili Taasisi za Kikristo zilizokuwa chini ya Serikali
zirudishwe na kuwa chini ya Kanisa kama ilivyokuwa awali.
4: Umiliki wa Balozi Mahalu wa shamba la hekta 500 kandokando ya
barabara iendayo Bagamoyo haukumfurahisha aliyekuwa Bosi wake enzi zile
kama Waziri wa MFAIC. Sasa hivi shamba lote limemegwa na kuwa sehemu ya
EPZ ya Bagamoyo.
5: Kama michezo michafu iliyochezwa kwenye majengo ya Ubalozi wetu
Burundi, Khartoum na nchi nyingine, Balozi Mahalu alishitulia NJAMA za
kuuzwa kwa jengo la makazi ya Balozi pale Roma. Njama hizi zilibuniwa na
maofisa wa MFAIC.
Balozi Mahalu alihakikisha kwamba suala la uuzwaji huo kiholela
limefikishwa kwenye vyombo vya sheria kule Italia na kufanikiwa
kurudisha umiliki wa hilo jengo kwa serikali ya Tanzania.
Na hapo pia balozi Mahalu alijiongezea MAADUI ambao wamedumu hadi leo.
Pata docs JF
No comments:
Post a Comment