JE, Nchi hii kuna Raia wa Tanzania na Raia wa CHADEMA?

 Wana jamvi,
Kama tunakumbukuka hivi karibuni kulitokea Mlipuko wa Malaria Muleba uliohatarisha maisha ya watoto na akina mama wajawazito. Tunashukuru serikali iliona hilo na kutuma timu ya madaktari kwenda kuokoa maisha ya wagonjwa, pia kuwafariji walioondokewa na ndugu zao kwa malaria.
Katika hili Serikali iliona hakuna jinsi zaidi ya kumtuma Waziri @anna tibaijuka kwenda kwa ndege ya Serikali akiwa mwenyewe kwenye ndege kujionea hali na kuwafariji ndugu waliokumbwa na mlipuko ule wa Malaria. Hapa serikali inaweka bayana kuwa Malaria ni ugonjwa wa Dharura ambao ulihitaji attention ya serikali. Kwa hili, pamoja na kwamba serikali ilitumia gharama kubwa ambayo ni kodi za watanzania walalahoi kwa waziri ambaye siyo daktari wala hakuenda Muleba kuwabeba wagonjwa kwa ndege, bado watanzania tulijiaminisha kwamba huu ndiyo uwajibikaji wa serikali yetu tukufu kwa wananchi, bila kuangalia gharama zilizotumika.

 Wana jamvi,
 Katika kumbukumbu zetu sahihi, katikati ya Mwezi June kulitokea Mlipuko Bomu na Matumizi ya risasi za moto katika Mkutano wa CHADEMA, wakuhitimisha kampeni zake za udiwani Arusha. Mlipuko ule uligharimu maisha ya watu wanne, na kuwajeruhi wengine zaidi ya sabini.
Katika mlipuko ule tulitarajia Serikali kuwasaidia hasa kuwafariji wafiwa na ndugu za wagonjwa, pamoja na CHADEMA ambao kimsingi ndiyo walikuwa waathirika wa mlipuko ule. Lakini cha ajabu mpaka leo hii hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyejihusisha na ishu ya Arusha zaidi ya kufanya kisiasa, kwa kutoa lugha za matusi na kejeli kwa raia wa Arusha.
Rais wetu Kikwete yupo kimya, tokea mlipuko ulipotokea mpaka leo hajatoa tamko lolote.
Watanzania tunajiuliza kama kweli Serikali inawathamini watu wake wa Arusha.
Sasa swali kwa Serikali, Kama Serikali iliweza kutuma Ndege yake kwa dharura kwenda Muleba kuwafariji watu, JE, kwanini imeshindwa kufanya hivyo kwa watu wa Arusha? Au ndiyo tuseme waathirika wa Mlipuko wa Bomu Arusha ni Raia wa CHADEMA?

No comments:

Post a Comment