KAMPUNIya mbunge wa
Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono inadaiwa kulipwa na T anesco, takriban
shilingi 18 bilioni kwa huduma ya ushauri, MAWIO imegundua.
Nyaraka ambazo
gazeti hili limeona zinaonyesha kuwa tayari kampuni ya Mkono imetumia kiasi
hicho kutoka shirika la umeme 'linalolegalega kifedha.
Mkono na kampuni
yake ya Mkono & Co. Advocates ya jijini Oar es Salaam, amekuwa mshauri wa
kisheria na wakili wa Tanesco tangu Mei 1995.
Nyaraka zinaonyesha
kuwa shilingi 18 bilionj zimelipwa kwa ushauri na utetezi ambao kampuni ya
Mkono imefanya katika minyukano ya kudaiana kati ya T anesco na kampuni
'nyingine ya umeme, Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Hivi sasa uhusiano
wa Tanesco, kampuni ya umeme ya serikali na kampuni ya Mkono, umekuwa wa kilio
kama mawasiliano ya ndani yanavyoonyesha.
barura ya Jenerali
Robert Mboma, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, ambaye inalalamikia
' maturnizi ya rnabilioni ya shilingi ya kampuni ya Mkono, tena bila mafanikio.
Barua ya Mboma ya l0 Septemba 2013; kwenda kwa Mkono, inalalamikia matumizi ya
kiasi hicho cha fedha katika mashauri ambayo yamechukua muda mrefu na bila
kuleta tija. Barua yenye Kumb. Na. SEC.427/IPTU9/2013; ambayo imebeba kichwa
cha maneno . kisemacho, "Ushauri ambao kampuni yako imetoa kwa Tanzania Electric
Supply Company Limited," imenukuliwa kwa Waziri wa Nshati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo. "Kwa sasa, kulingana na kumbukumbu tuiizonazo,
kampuni yako imekwishatumia takribani Sh. 18 bilioni kama gharama za ushauri
katika kusimamia suala hili kufikia Aprili 2013," anaeleza Jenerali Mboma.
Anasema, "Hiki ni kiasi kikubwa mno cha
fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kuwekezwa kwenye miradi mingine ya
uzalishaji kwa manufaa ya Watanzania wote."
Kana kwamba hiyo
haitoshi, Mboma anasema, "Tanesco inataka ieleweke kuwa inasikitishwa na
namna kampuni yako ilivyotoa . ushauri wa kisheria kuhusiana na mivuteno
iliyohusu Mkataba wa mauziano (PPA) wa tarehe 26 Mei 1995 kati yetu na IPTL,
kwa vile ulivyotushauri na katika kuisimamia kesi tangu'ilipofunguliwa mwaka
1998."
Tanesco sasa
inatuhumu kampuni ya mkono kutoishauri vizuri hadi kupoteza kesi yake dhidi ya
IPTL. Kesi ambayo Tanesco inasema imeipoteza, kwa kutoshauriwa vizuri inahusu
mkataba wa kununua umeme - Power Purchase Agreement (PPA) wa 26 Mei 1995.
Kampuni ya IPTL
ndiyo kampuni ya kwanza ya nje kuingiza . mitambo ya kuzalisha umeme wa dharula
nchini. Mitambo yake inatumia mafuta mazito (Industrial Oiezel Oil- 100); jambo
ambalo linasababisha urnemeinadzalisha kuwa ghali kuliko ule wa kuzalisha kwa
kutumia gesi na, au maji.
Taarifa kutoka
ndani ya Tanesco zinasema, mbali na malipo Mkono, kampuni ya IPTL hukomba kiasi cha sh 1.8 bilion kila mwezi zikiwamalipo kwa
gharama za kuweka mitambo yake nchini - Capacity Charge.
Mtoa taarifa kutoka
ndani ya serikali anasema, kwa kuwa Tanesco inakabiliwa na ukata mkubwa wa
fedha kutokana na mikataba ya kinyonyaji ya umeme, serikali hutoa kila mwezi,
kiasi cha Sh. 3.8 bilioni kuwezesha shirika hila kununua mafuta ya kuendesha
mitambo ya dharula .
Gazeti
halikufanikiwa kumpata Jenerali Mboma. Mara zote simu yake ya mkononi ilijibu
kuwa haipatikani.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema hana taarifa ya suala hilo. Alitaka
mwandishi amuonyeshe kwanza mawasiliano yaliyofanywa kati ya pande hizo mbili. Alipoelezwa
gazeti limeona nyaraka hizo zilizonakiliwa kwa waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo, Maswi alisema, " ... siwezi kulijua suala hilo."
Naye Mkurugenzi Mtendaji Tanesco, Felchesmi Mramba, hakupatikana. Meneja
Uhusiano wa T anesco, Badra Masoud alisema hawezi kuzungurnzia suala hila kwa
kuwa ni jambo linalohusu Bodi.
ilipokewa na mtu aliyejitambulisha ni dereva
wake. Alisema basi wake yuko kwenye kikao.,Aliomba apigiwe baadaye.
Alipoitwa baadaye,
dereva huyo alisema, “. .. bado yuko kwenye kikao, Alishauri atumiwe ujumbe ili
. ampatie.
Gazeti lilituma
ujumbe kwenye simu ya Mkono ambao ulisema, "Tunataka kujua msimamo wako
kuhusu malalamiko ya T anesco kuwa kampuni yako ya uwakili imetumia 18 kwa kazi
za ushauri na kusimamia kesi dhidi ya IPTL ... " Mkono hakujibu ujumbe
huo. .
Kampuni ya Mkono
imo katika umoja na kampuni ya SNR Denton. Imeelezwa kuwa umoja huo wa kampuni
unaundwa na zaidi ya wanasheria 1,100 wa Uingereza, Marekani, Canada na
Tanzania; na una makao makuu jijini London, uingereza.
Tanesco limeeleza
kwamba lilishauriwa na wanasheria wa Mkono & Co. Advocates kuwa lina hoja
za msingi kudai urekebishaji wa kiwango cha bei na kwamba "Tanesco
watapaswa kudai kiasi kitakachokuwa kimezidi kutokana na ankara za IPTL
zilizotozwa baada ya maamuzi.
" ...
ulitushauri tutoe indhari ya madai ya ankara za ziada kwa IPTL. Tukapinga
ankara za malipo zilizohusu gharama za kuweka mitambo - Capacity Charge. yote
haya yalifanywa kwa kuzingafia ushauri wako," imeeleza barua ya Mboma kwa
Mkono na kwamba hatua hiyo haikufanikiwa.
Katika barua , Tanesco
inalalamikia kampuni ya Mkono kwamba pamoja na kutoa ushauri 30 Juni 2004 kuwa
shirika hilo lina hoja za msingi na halali kuomba urekebishaji wa bei ya umeme
na kurudishiwa malipo ya ziada, lakini 4 Oktoba 2012, Mkono alikwenda na
mtizamo tofauti.
"Katika barua
yako ya 4 Oktoba 2012, umesema kuna uwezekano mdogo sana wa kushinda kesi hiyo
kutokana na kugundulika kwa baadhi ya nyaraka zilizodhoofisha utetezi
uliotolewa mapema na shirika," barua ya Mboma inaeleza.
Inaongeza,
"Ulitushauri kwa hoja nzito kuwa tupiganie usuluhishi na Benki ya Hong
Kong - SCB HK au kampuni yako ielekezwe zaidi kuwasilisha ombi la kukataliwa
kwa uamuzi unaoinufaisha benki hiyo,"Mboma anaeleza mkono
kwa njia ya malalamiko.
Barua ya shirika
hila inajibu maelezo ya Mkono ya kutaka malipo ya zada ya fedha kwenye· kesi
hiyo wakati Tanesco haioni manufaa ya malipo hayo.
Wakati wote wa
mgogoro, fedha zilizokuwa zinabishaniwa mahakamani, ziliingizwa kwenye .
akaunti maalum iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kutokana na mfumo
huo wa kubishania ankara, IPTL ilifungua malalamiko mbele ya Taasisi ya
Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) wakitaka kupatikana tafsiri halisi
ya eneo hila . kulingana na mkataba wa mauziano ya umeme.
Katika hatua hiyo,
Tanesco inalalamikia kampuni ya Mkono ambayo iliiwakilisha mpaka pale shauri
hila li!ipofutwa kwa manufaa ya IPTL kutokana na amri iliyotolewa 19 Agosti
2010. Kwa barua ya kampuni ya Mkono ya 4 Oktoba 2010, Tanesco inajulishwa
kuhusu nia ya benki ya Standard Chartered Hong Kong (SCB HK) kufungua ombi la
usuluhishi baada ya IPTL kuacha kuendelea kwa shauri. Matokeo yake, mbali ya kuihakikishia
Tanesco kuwa itashinda, ikashauri pia shirika lielekeze kampuni hiyo ya uwakili
kuendelea kutaka kusimamishwa kwa usajili wa malalamiko ya SCB Hlvrnbele ya
ICSID kwa hoja kwamba SCB HK haina uhalali katika suala hilo. T anesco walitoa maelekezo
hayo kwa ma~akili wa Mkono~', . Hata hivyo, T anesco inalalamika kuwa mawakili
hao walishindwa kuzuia SCB HK kusajili malalamiko yake na hatimaye, "Ombi
(letu) kuhusu suala hilo lilitupwa." "Usajili wa SCB HK ulikubaliwa na
ICSIQ, na ukasikilizwa kama ulivyopangwa," imesema T anesco katika barua
yake kwa kampuni ya Mkono.
Mara tu usikilizaji wa usuluhishi , ulipofungwa Aprili 2013,
Tanesco inasema kampuni ya uwakili ya Mkono ilishauri shirika kufungua ombi la
kucheleweshwa tamko la ICSID lakuipa SCB HK ushindi mpaka kwanza kusubiri
uamuzi wa ombi la SCB HK lililokuwa likiendelea kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania. "T anesco ilizuia,
lakini pia; ilishindwa. ICSID ilisema kuwa itatoa tamko lake ndani ya miezi mitatu,"
barua ya Mboma inaeleza. Tanesco, mbali na kulipa mabilioni hayo ya shilingi
kwa ushauri, imekuwa ikilipa fedha nyingi kwa makampuni yanayodai kutoa huduma
za kisheria, ikiwamo kesi kati ya shirika hilo na makampuni ya Richmond Development
Company (DRC), Dowans Holding na Dowans Tanzania Limited. Kuibuka kwa taarifa
hizi kumekuja miaka sita baada ya Mkono kutajwa na kiongozi mkuu wa upinzani
nchini, Dk. Willibrod Slaa kuwa ni miongoni mwa watuhumiwa 11 wa ufisadi
nchini. Mbele ya umati mkubwa, kwenye mkutano wa hadhara katika Viwanja wa
Mwembeyanga,' Temeke, Dar es Salaam, Dk.
Slaa . alisema Mkono, kupitia kampuni yake ya Mkono & Co. Advocates amekuwa
akilipwa malipo makubwa, hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia, ambamo BoT inadaiwa
jumla ya Sh. 60 bilioni. Ok. Slaa alisema, kwa mujibu wa Mkaguzi na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali (CAG), kampuni ya Mkono tayari imelipwa zaidi ya Sh. 8.1 bilioni,
fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahekamani Malioo havo wakati huo
valikuwa sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa BoT.
Chini ya Kanuni za
Malipo ya Mawakili na Uamuzi wa Gharama za Kesi za mwaka 1991 (T angazo la
Serikali Na. 515la - I " 1995), ki':Vango cha malipo ya . mawakili katika
kesi ambaao fedha : inayodaiwa ni zaidi ya Shs 18 milioni, kitakuwa asilimia
tatu. Kwa kufuata masharfi ya sheria hii, kampuni ya Mkono ilipaswa kulipwa Sh.
1.8 bilioni. Aidha, kampuni ya Mkono inatajwa katika taarifa ya uchunguzi
kuhusu tuhuma dhidi ya makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., ' Centrepoint
Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd., yanayomilikiwa na V. G. Chavda
kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha za Debt Conversion Procramme. . '
No comments:
Post a Comment