Hii ni sensa ya tano(05) tangu Tanzania ipate uhuru wake.Wananchi
wanaombwa wawe tayari kujibu maswali kuanzia 1-37 au 1-62;hii ina maana
kwamba kuna watu watakaojibu maswali 37 na kuna wengine watakaojibu
maswali 62, na hii ni kwa mujibu wa dodoso la sensa 2012.
Zoezi hili litaanza usiku wa tarehe 25/08/2012 kuamkia tarehe 26/08/2012
na litadumu kwa siku saba (07).Sensa hii ni muhimu kwa mtu mmoja mmoja
na kwa tathimini ya mipango ya nchi kwa ujumla;na sensa hii ni muhimu
zaidi ya hizo sensa nne(04) zilizopita.
Watakao hesabiwa ni wale wote wataokuwepo ndani ya nchi katika kipindi
chote cha zoezi hili nyeti kitaifa;na mtu anahesabiwa mara moja tu na
siyo vinginevyo.
No comments:
Post a Comment