Naskia kuna malalamiko kuwa Kanda ya ziwa licha ya kuwa Migodi yote ya
Dhahabu iko kule hakuna hata international airport, Mwanza airport ni
kama shule ya kata ni kweli?
Nasikia kuna Malalmiko Rocky City Mwanza, Kikwete hadi December 2011
hajaleta hata Sh. kumi ya ruzuku ktk Jiji wakati hadi leo alitakiwa awe
ameshatoa 40Bilioni ili kuwakomoa kwa kuwapiga chini ktk Uchaguzi ni
kweli?
Nasikia kuna malalamiko, yakuwa lile Jiwe maarufu la Bismack pale
Kamanga Ferry lililokuwa ktk noti ya Tsh. 1000 likiwa na sahihi ya
Mramba na Balali pia wameiondoa na kuweka kilima cha pale Gairo kikiwa
na sahihi ya Mkulo na Ndulu, ni kweli?
Naskia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa licha ya kuwa na watu 16mil
kati ya 45mil Tz, Katiba imejadiliwa Dodoma, Dar na Zanzibar, hawataki
kabisa kuwashirikisha kisha wanataka CCM muwapiguie kura, ni kweli?
Naskia Kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa asilimia hamsini
ya wasomi wote tanzania wanatoka kule hakuna hata chuo kikuu hata
kimoja cha serikali ni kweli?
Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa na madini
yanayoweza zalisha Cement yako pale Shinyanga hakuna hata mpango wa
kujenga kiwanda licha ya kuwa 2005 mliahidiwa ni kweli?
Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa mkoa mpya wa Simiyu umeomba
ile barabara inayopita serengeti mmeomba ipitie Lamadi, bariadi kuja
Hydom na kuunga Babati naskia wamekataa ni kweli?
Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa kuna hakuna viwanda licha ya
kuwa mna bidhaa nyingi lakini vinajengwa vyote pwani eti msafiri mkaombe
vibarua Kibaha na bagamoyo ni kweli?
Nasikia kuna malalamiko kanda ya ziwa kuwa ili bandari ya nchi kavu
Isaka-Shinyanga vijijini nayo imekufa ili kuimalisha ajira ya pwani na
kuanzisha bandari mpya ya nchi kavu Chalinze ni kweli?
Naskia kuna malalamiko kuwa wilaya nyingi za zamani kama Musoma
vijijini,Shinyanga Vijijini hazina hata makao makuu lakini baadhi ya
zilizoteuliwa juzi juzi tuu zimejengwa vizuri ile mbaya ni kweli?
Sasa kama ni kweli mnangoja nini- Hameni wote Si Si EM inaonekana wanachumia kwenu halafu wanawekeza kule Chalinze
Source: JF..http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/143489-nasikia-malalamiko-kanda-ya-ziwa.html
No comments:
Post a Comment