Kama jina lilivyo Usalama waTaifa.
Ni chombo kilichoundwa ili kuhakikisha njama zozote za kuturudisha
katika mikono ya wakoloni, za nje na za ndani, zinakomeshwa kabla
hazijaweza kufanikiwa. UWT kazi yake namba moja ni kulinda Uhuru wa
Tanzania kwa kuvunjilia mabali njama za wahaini wanao taka kuua nguvu za
uchumi. Kazi yao nyingine kubwa ni kumlinda Rais wa Jamhuri dhidi ya
maadui wa ndani na nje. Kutokana na WT kuwepo kwao Ikulu muda mwingi na
ukweli kwamba rais wetu hana maadui wa ndani na wa nje kwa sabau
amewaridhisha maadui wote ipasavyo hivyo hakuna anayetishia maisha
yake! Usalama wa taifa wamekuwa wakifanya kazi ya kuhakikisha kwamba
wanalinda kwa gharama yeyote Udhaifu wa mkuu. Hata ikibidi kuua. Lolote
analosema na kuwaza mkuu hata kama ni utumbo wa kunuka wa FISI wao
hujitoa muhanga na kuhakikisha halipingwi wala kubezwa.
Miaka ya hivi karibuni usalama wa Taifa umekuwa reduced role yake to
infinitly small na kuassume kazi ya Group4 au Ultimate Security. Na sasa UWT ume kuwa reduced even more sasa kuwa Genge la Maharamia wauaji kwa niaba ya chama tawala CCM. UWT are functioning as CCM attack Dogs. This is the biggest shame ever to UWT.
Wakati mwingine hutumika kuiba kura au kuingiza masanduku Fake. Sijui
kuiba kura nakuwa mbwa wa CCM kunasaidia vipi kuimarisha Uhuru wa
Tanzania??
Kuteka watu mashuhuri wanao ibana serikali na kuwapiga kipigo cha mbwa
mwizi huku wakitumia Nembo ya Ikulu na jina na Rais wa serikali ya CCM
ni upeo wa juu kabisa wa Uharamia wa serikali ya CCM na vyombo vyake
vya usalama na hata Mahakama.
Vyombo vya kulinda uslama wa wananchi vinapogeuzwa na Wanasiasa Dhaifu
wa CCM ili kulinda udhaifu wao kwa Gharama ya Damu na hata uhai wa
waTanzania ni dalili moja kubwa kwamba hila zote za Utawala wa CCM
zimegusa Glass ceiling na kufikia mwisho wake. Ni dalili nyingine kubwa
kwamba kikombe cha matendo yao maovu kimejaa na kuanza kufurika. Pia ni
dalili moja kwamba saa ya upatilizo wa ghadahbu ya uovu wao imefika na
uvumilivu wa wananchi umefikia kikomo. Ni Dalili kwamba serikali
imeingia HOFU na woga MKUU kiasi cha kudhani kuua wasemaji wakuu kutaua
matatizo yanaikabili kwa udhaifu na Ulegevu wake.
Serikali
siku zote hutumia utajiri na uwezo wake kuhakikisha kwamba inatoa
huduma za afya bora ili kurefusha maisha ya rasilimali yake kuu yaani
watu, hasa watu wale walioelimika vya kutosha kama Dr Ulimboka. Ukiona
serikali inatumia Jeshi lake la Polisi au UWT kuua rasilimali yake kuu,
watu, kwa visingizio vya UNATUSUMBUA, UNATUCHEZEA,UNAJIFANYA UMESOMA??
Ujue serikali hiyo ni MFU Imebanduka gamba la kusetiri uovu wake na Kifo
kinaizengea serikali hiyo kwa hamu.
Hii si mara ya kwanza kwa Usalama wa Taifa chini ya maagizo ya Ikulu
kuteka watu kisha baadaye watu hao kukutwa wamekufa katika misitu
inayozunguka ukanda wa Dar na Pwani. UWT wamekwisha ua watu wengi
wanaoipa ukweli serikali ya CCM na hata wafanya biashara na kudhurumu
mali zao kisha kutupa miili yao huko misituni. Huu ni uharifu unaolindwa
na Chama Cha mapinduzi na Ikulu ili kudmisha Udhaifu na ulegevu wake.
Watu huuawa kwa sababu mara zote mtu akifa chini ya mkono wa UWT kundi
la watu hufaidika kwa kupewa malipo makubwa ya mamilioni ya fedha, vyeo
na hata sherehe za kupongezana kwa bia na umalaya.
Kubwa kuliko yote, mauaji haya ya kupangwa na UWT kwa amri a Ikulu
huhakikisha kwamba yanalinda maslahi ya wachache wanodumisha Ufisadi,
Rushwa, Wizi,Uhaini dhidi ya Jamhuri na Ushiriki wao katika kuiuza
Tanzania kwenye Mashirika makubwa ya kimaifa ambayo ndiyo Muhimili mkuu
wa Ukoloni mambo leo.
Dr Ulimboka kwa standard ya serikali ya CCM ni mtu asiye takiwa kabisa
kwa sababu anafichua maovu ya serikali ya CCM katika idara ya Tiba. Dr
Ulimboka ni mtu anaye amsha hisia za waTanzania kudai uwajibikaji wa
serikali kwa wananchi.
Serikali ya CCM haiko tayari kabisa kuambiwa ukweli wa udhaifu wake wa kugeuza nchi Shamba la BIBI.
Serikali ya CCM inakumbatia wahalifu wote na mharamia wauaji na wapora
mali za Watanzania. Kwa Uovu wake Inatoa Ulinzi mkubwa kwa watenda Maovu
ambayo ndiyo chanzo cha kuzorota na kudidimia kwa huduma ya afya
Tanzania NA UCHUMI KWA UJUMLA.
Naamini kabisa juhudi za kumnunua Dr Ulimboka zilishindikana kabisa.
Naamini kabisa vitisho dhidi ya Dr Ulimboka vilishindika kabisa.
Naamini aina yeyote ya mkwara na uongo wa kutupwa kama divide and rule dhidi ya Dr Ulimboka vyote viishindikana kabisa.
Baada ya kushindwa kuvunja moyo wa ARI wa Dr Ulimboka Amri kuu ilitoka
Ikulu ya kummaliza na kuhakikisha kilanga chake kinazimwa milele daima.
Hapo ndipo Majambazi waajiriwa wa UWT na Ikulu walipochukua Gari jeusi
na kumbeba kwa nguvu Dr Ulimboka kwenda huko machakani huku wakiamini
kwamba hii ndo ingekuwa safari yake ya mwisho.
These F*%ken suckers didn't know that God rules everything including death.
They thought they killed him, now they are dying to cover their evil foot prints
They thought it was over,now they have to face a new bigining and the truth
Dr Ulimboka bado hajamaliza kazi yake, na saa yake ya kurudisha namba bado haijafika.
Vilevile Mungu kamzidishia Uhai ili maadui zake waaibike washindwe na kuangamia milele kwa uovu wao wenyewe.
Serikali ya CCM kwa muda wa miaka 50 imekuwa ikitumia kila hila
kuhakikisha kwamba sisi wananchi tunazidi kudumaa katika hali yetu ya
MSUKULE.
Waliwahi kutudanganya kwamba Ujamaa ni imani wakati wao wenyewe Imani yao ni fedha na Unyonyaji.
Waliua vyama vya ushiriki vyenye sura ya umoja na ujamaa wa kweli.
Waliwahi kutuambia Kilimo ndiyo uti wa mgongo. Walihakikisha kwamba
tunaamini kilimo duniani hulimwa kwa jembe la mkono, kulima kwa trekta
ni uvivu na uzembe, kisha wakaua hata hicho kiwanda cha majembe. Wakati
huo huo wenyewe kununua matrekta na kulima kilimo cha mashamba makubwa
huku wakiendesha magari makubwa ya zaidi ya $100,000.00
Wametumia katiba kunyanyasa watu na kutunyima Uhuru wa kujieleza.
Wanahonga wahariri ili wasiandike ukweli na wale wasio kubali hongo
wanamwagiwa tindikali machoni ili wasiandike tena.
Sasa wanatuambia nchi inafuata mkondo wa ubepari wakati katiba bado
inasema nchi hii inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Serikali ya
watu waongo na wahaini.
Uongo ukawashinda, wakaanza kutumia fedha.
Wananunua kura, wananunua watu wa kujaza katika mikutano yao iliyo jaa ujinga na matusi ya nguoni.
Wananunua watu wasigombee kupitia vyama vya upinzani.
Wananunua Majaji na kugiza watoe hukumu aina gani.
Wananunua hata haki za mama zao wazazi ili kudumisha UDHAIFU wao
Wanahakikisha fedha haziwafikiii walengwa ili hali duni ya huduma na ustawi izidi kuwabana wananchi.
Sasa wanateka watu na kuwapa kipigo cha kuua ili kudumisha Utawala wao.
Wanadhani watafanikiwa kwa kuua.
Washenzi Vihiyo wakubwa hawajasoma Historia ya dunia ikawaelea. DOLA HUSIMAMA KWA UPANGA HUENDA CHINI KWA UPANGA
Hivi serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni Wababe kuliko serikali ya Egypty iliyoongoza kwa Rungu la Chuma kwa zaidi ya miaka 60??
Serikali ya CCM ni Babe kuliko ile ya Gadhafi?
Kila
Siku CCM Wanajivunia AMNI na UTULIVU. Amani ya kuteka na kuua watu
kisha bila aibu wanasingizia eti kuna watu ndugu yao kafa kwa hasira
wamemteka Dr Ulimboka na kumpiga. Huu ni uongo unao faa kusemwa na
kupigiwa makafi kwenye kikao cha NEC ya CCM tu, maana huko ukisema
ukweli kazi huna.
Hivi Serikali ya CCM wandhani kuongea Kiswahili ndo kinga ya kufanya
vurumai isitokee?? Mbona wasomali wote wanaongea kisomali na wote ni
waislamu lakini nchi imesambaratika??
Ninyi Viongozi wa Chama Cha mapinduzi na wa Serikali ya CCM hakikisheni
mna pa kufikia huku Ughaibhuni ili siku ikifika msihangaike. Na ninyi
UWT mnaotumiwa kama vijiko vya Chips Ole wenu.
Source: JF
No comments:
Post a Comment