TAARIFA
KWA UMMA
Ninalazimika
kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani hotuba yangu
niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha
siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi
kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya
siasa hususani chama tawala CCM.
Kumetokea
sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa
ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama
ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote
katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda,
udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala
dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa
ikitafsiriwa.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya
mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema
Mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa
wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na
chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi
tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano.
Lengo
la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi
lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi
mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au
kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake.
Joshua
Nassari (MB)
Mei 09,
2012.
No comments:
Post a Comment