Method Kimomogoro amekamilisha na kuwasilisha mahakamani rufaa ya
kupinga hukumu iliyomvua ubunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema
huku akiainisha hoja 18 za kupinga kukata rufaa.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za kimahakama zilizopatika Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha, rufaa hiyo iliwasilishwa Ijumaa ya Mei 4, mwaka huu tayari
kwa ajili ya kuwasilishwa kwa msajili wa Mahakama ya rufaa Jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kusajiliwa.
Akizungumza ofisini kwake jana, Wakili Kimomogoro alithibitisha
kukamilisha na kuwasilisha rufaa hiyo mahakamani tayari kwa ajili ya
kupangiwa jopo la majaji wa kuisikiliza.Pamoja na hoja za rufaa, kitabu
hicho cha rufaa chenye kurasa 985 ina mwenendo mzima wa shauri,
vielelezo na viambatanisho vyote vilivyowasilishwa Mahakama Kuu.
“Kimsingi ni rai yangu kuwa mtukufu Jaji Rwakibarila (Gabriel) hakutolea
uamuzi mambo na hoja za msingi zinazofanya hukumu yake kukosa hadhi
kisheria, kuitwa hukumu, hayo ni miongoni mwa hoja za msingi
nilizoanisha kwenye rufaa niyowasilisha mahakamani juzi,” alisema Wakili
Kimomogoro.Kwa mujibu wa hati ya rufaa hiyo, hoja ya kwanza hadi nne
zinapinga uamuzi wa Jaji Aloyce Mjulizi aliyesikiliza shauri hilo katika
hatua za awali kwa kutupa pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande
wa utetezi kwenye kesi ya madai namba 13 iliyofunguliwa na wapiga kura
watatu waliopinga ushindi wa Lema.
Miongoni mwahoja hizo ni kuwa wadai, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy
Kivuyo hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo kwa sababu hakuna
haki yao iliyovunjwa kisheria kama wapiga kura.Wakili Kimomogoro
aliyemwakilisha Lema na mawakili wa Serikali, Timon Vitalis na Juma
Masanja walidai aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Dk Batilda Burian ndiye alikuwa na haki kisheriakulalamikia
ushindi na maneno ya kashfa yanayodaiwa kutolewa dhidiyake na Lema.
Hoja ya tano hadi 18 zinapinga hukumu ya Jaji Rwakibarila ambapo katika
suala la hukumu yake kukosa hadhi kisheria, wakili Kimomogoro anadai
hakutolea maamuzi athari za wadai kushindwa kuwasilisha mahakamani CD
zinazomwonyesha Lema akitoa maneno ya kashfa na udhalilishaji walizodai
kuwa nazo katika hati yao ya madai.
Kimomogoro anadai Jaji alikosea kwa kutotumia hata kesi moja kama rejea
kati ya kesi kadhaa zilizotajwa na mawakili wa pande zote mbili za wadai
na wadaiwa.
Jaji Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya
Sumbawanga pia anadaiwa kukosea kisheria kwa kukubali na kuegemea
ushahidi wa mdomo pekee katika hukumu yake bila kuwepo ushahidi wa
mazingira, Video wala maandishi kuunga mkono ushahidi wa mdomo.
Mrufani pia anadai Jaji alikosea kwa kutumia viwango na vigezo tofauti
kwa mashahidi wa upande wa wadai na utetezi kwa kukataa ushahidi wa
Leman na mashahidi wake kwa madai kuwa walikuwa na maslahi kwa sababu ni
wanachama na viongozi wa Chadema lakini akakubali ushahidi wa wanachama
na viongozi wa CCM kutengua matokeo.
Hoja nyingine ni kuwa hata kama Lema angetiwa hatiani kwa madai
yaliwasilishwa mahakamani, bado Jaji hakustahili kutumia kifungu cha 114
cha sheria za uchaguzi kuripoti uamuzi wake kwa Mkurugenzi wa uchaguzi
kwani makosa hayo hayahusiani na vitendo vya rushwa wala jinai ambavyo
humzua aliyehukumiwa kupiga kura wala kugombea uongozikwa miaka mitano.
KWA HISANI YA GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment