NSSF imeanza zoezi la kuwabembeleza/kulazimisha wateja wake wakubwa
[waajiri] kutoa mchango yao ya kila mwezi kabla ya wakati.Ni kawaida
waajiri kupeleka michango ya kila mwezi mmoja nyuma[mfano mshahara wa
mwezi tano michango yake inatakiwa ipelekwe mwezi sita],sasa NSSF
inawataka waajiri wakubwa [waajiri wenye idadi kubwa ya wafanyakazi]
kupeleka michango ya wafanyakazi mwezi mmoja mbele au mwezi huu wa sita
ili kukabiliana na hali mbaya ya fedha inayoliandama shirika hilo la
wafanyakazi nchini.
Taarifa toka chanzo cha uhakika ndani ya shirika hilo zinadai serekali
imechota fedha toka NSSF kwaajili ya kugharamia mishahara ya watumishi
wake baada ya chanzo chake muhimu cha mapato TRA kushindwa kupata fedha
za kutosha kulipa mishahara ya watumishi wa serekali pamoja na shughuli
nyingine muhimu.
Zipo taarifa za uhakika serekali ina mkakati wa kuwalazimisha wanachama
wote wa NSSF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kutokulipwa mafao
yao hadi wafikishe umri wa kustaafu.Mkakati utasaidia kukabilia na
upungufu mkubwa wa fedha unaotarajiwa kutokea kwakuwa fedha zinazochotwa
na serekali hazitarajiwi kurejeshwa.
Source: JF
No comments:
Post a Comment