UCHUNGUZI
KUHUSU JARIBIO OVU LA KUCHOMA MOTO OFISI ZA CHADEMA ARUSHA.
Jana 3/12/2013 jaribio baya lilifanyika dhidi ya kuchoma ofisi ya CHADEMA ya Kanda ya Kaskazini na Mkoa wa Arusha .
Jana 3/12/2013 jaribio baya lilifanyika dhidi ya kuchoma ofisi ya CHADEMA ya Kanda ya Kaskazini na Mkoa wa Arusha .
Hata
hivyo Jeshi la Polisi lilifika kwa ajili ya uchunguzi wa awali na Chama
kilielekeza Kitengo chake cha Usalama na Ulinzi kuanza kufuatilia jambo hilo
kwa kina ili kubaini wahalifu wa jaribio hilo baya . Taarifa ambazo tumepokea
mpaka sasa ni taarifa muhimu ambazo tunahamini zitaisadia Jeshi la Polisi
katika uchunguzi wake.
Tumepeleka
majina ya Watu ambao taarifa zetu za kina zinaonyesha wanahusika na tukio hili
takribani wasiozidi watano na ni imani yetu kuwa Jeshi la Polisi litachukuwa
hatua muhimu katika uchunguzi wao huku Chama tukiwa tiyari kabisa kutoa
ushirikiano wa dhati katika uchunguzi wa kina na wakitaalaamu ambao utaweza
kuthibitisha udadisi wetu na uchunguzi wetu ili kuponya Taifa letu .
Hata
hivyo Chadema kinalitaka Jeshi la Polisi kutokufanya Siasa katika jambo hili
kwani ni muhimu wakaelewa kwamba kupuuza uchunguzi wa jambo hili ni hatari kwa
Mkoa wa Arusha na mustakabali wa Amani ya Taifa letu . Chama katika utafiti
wake kimebaini kuwa miongoni mwa washukiwa katika tukio hili wamekuwa ni Vijana
ambao wamekuwa wakifanya kazi na Polisi katika jitihada za kuhujumu Chadema na
hivyo kunaleta mashaka makubwa juu ya uchunguzi wa jambo hili kama utafanyika
kwa ufasaha na weledi wa hali ya juu kwa majina ambayo Chama imemkabidhi
Kamanda wa Polisi Mkoa .
Hata
hivyo katika uchunguzi wake Chadema inasikitishwa sana na kitendo cha Serikali
kumpatia mmoja wa washukiwa umiliki wa silaha aina ya bastola wakati Mtu huyo
akiwa na rekodi ya kuwa na kichaa cha mara kwa mara .
Chadema
Kanda ya Kaskazini inawataka Wanachama wake na wafuasi watulie kimya bila
kutafakari aina yeyote ya kisasi kwa jaribu hili baya ili kutoa fursa njema kwa
Viongozi wao na Jeshi la Polisi ili kuwabaini Watu hawa waliotaka kuteketeza
Ofisi ya Chama kwa moto . Lakini pia Chadema inamshukuru sana na kumpongeza
mmiliki wa nyumba hiyo kwa kutambua majaribu ambayo tumepitia wakati huu kwa
kukubali kurekebisha nyumba ambayo ni ofisi yetu kwa gharama zake mwenyewe kama
sehemu ya kuheshimu jitihada za kushinda hofu na woga unaotaka kupandikizwa
miongoni mwa jamii yetu .
NANYARO E.J.
Mwenyekiti
Wilaya
4/12/2013
4/12/2013
No comments:
Post a Comment