Kuhusiana na meli za Irani: soma taarifa ya Bernard Kamilius Membe.
Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha
bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili
zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. Tanzania imewaarifu nchi
zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na
kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa kuzingatia
uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa
kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala
wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran, Balozi
wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya utafiti na
ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara moja.
Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli hizo.
Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio 1920 la UN
Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani. Tunafurahia
mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo linalogusa maslahi
ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani (Muungano), tujihadhari
na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja kama taifa. Nchi kwanza!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment