Leo asubuhi sheikh ponda amepinga kauli ya mufti aliyoitoa jana akiagiza
waislamu kushiriki ktk sensa ya mwezi agosti mwaka huu. akihojiwa na
redio imaan iliyopo morogoro, sheikh ponda amesema kuwa bakwata ni moja
ya taasisi za kiislamu hivyo mufti hawezi kuamua peke yake bila
kuwashirikisha wajumbe kutoka taasisi nyingine.
"tulikutana dodoma na waziri wassira tukiwa wajumbe wa taasisi zaidi ya
10 za kiislamu, bakwata ikiwa moja wapo. msimao wetu ulikua mmoja kuwa
hatutoshiriki sensa hadi yafanywe mambo mawili. la kwanza kipengele cha
dini kiwekwe kwenye dodoso. la pili tume ya taifa ya sensa iwe na
mchanganyiko wa wajumbe waislamu na wakristo. waislamu kwenye tume ni
20%." alisema ponda.
alipoulizwa nini kitaendelea akasema kuwa taasisi zote zinakutana leo na
leo ama kesho watafanya press conference ili kuwaeleza watanzania
maazimio yao. "Mufti amejidhalilisha. nina imani waislamu watafuata
maelekezo yetu. mufti ataonekana jinsi asivyo fuatwa na kusikilizwa na
waislamu wengi."
source: JF
No comments:
Post a Comment