SERIKALI: Lulu ana zaidi ya miaka
MAWAKILI WA SERIKALI WAMKAANGA LULU
MAWAKILI wa Serikali jana waliwasilisha vielelezo Mahakama kuu
kuthibitisha kwamba umri wa msanii wa filamu Elizabert Michael ni zaidi
ya miaka 18.Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na
mawakili wawili; mmoja wa Lulu na mwingine wa Serikali ambao hawakutaka
kutajwa, zimeeleza kuwa vielelezo hivyo vimewasilishwa jana mahakamani
hapo.
Habari zimeeleza kuwa moja ya vielelezo hivyo vya Jamhuri ni Mkanda wa
video aina ya CD, yenye mahohjiano kati ya mshtakiwa huyo na mtangazaji
mmoja nchini.
"Vingine ni maelezo ya mshtakiwa huyo aliyoyatoa polisi wakati
alipohojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, maombi ya hati ya kusafiria
(Passport) na maombi ya leseni ya udereva, alisema mmoja wa mawakili
hao.
Awali vielelezo hivyo walitakiwa kuviwasilishwa juzi, lakini
ilishindikana na badala yake vikawasilishwa jana.
Baada ya vielelezo kesi hiyo itasikilizwa Juni 25 mwaka huu. Lulu
anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki
dunia nyumbani kwake Sinza, April 7, 2012.
Hata hivyo umri wake umezua utata baada ya mawakili wake wanaomtetea
kudai kuwa bado ni mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama
hati ya mashtaka inavyoonyesha.
Hivyo mawakili hao walilazimika kuwasilisha maombi mahakamani kuiomba
mahakama iruhusu ufanyike uchunguzi wa umri sahihi wa mshtakiwa huyo na
ikiridhika kuwa ni mtoto basi kesi yake iendeshwe kwa misingi ya kesi za
watoto wanaokinzana na sheria ili kulinda maslahi yake.
Juni 11, 2012 Mahakama Kuu ilikubali yenyewe kufanya uchunguzi huo kwa
lengo la kubaini usahihi wa umri wa mshtakiwa huyo na ikaziagiza na
kuzipangia tarehe pande zote katika kesi hiyo kuwasilisha mahakamani
hapo vielelezo watakavyovitumia katika hoja zao.
Jopo la mawakili wanaomtetea Lulu likiongozwa na Kennedy Fungamtama Juni
13 waliwasilisha mahakamani hati za viapo vya wazazi wake na vielelezo
vingine kikiwemo cheti cha kuzaliwa na cha ubatizo vinavyoonesha kuwa
bado ni mtoto.
Lakini taarifa zilizopatikana mahakamani hapo zinaeleza kuwa vielelezo
vilivyowasilishwa na Jamhuri vinaonesha kuwa mshtakiwa huyo ni mtu mzima
kwa kuwa kwa mujibu wa vielezo hivyo ana umri zaidi ya miaka 18.
Viapo vya wazazi wa mshtakiwa huyo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na
Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Peter Kibatala
ambaye ni mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu vinaeleza kuwa mshtakiwa
huyo ana umri wa miaka 17.
Viapo hivyo ambavyo Gazeti hili limefanikiwa kuviona ni kiapo cha mama
yake Lulu Lucresia Augustin Kalugila, mkazi wa Dar eS Salaam na kiapo
cha baba mzazi Michael Kimemeta, mkazi wa Moshi.
Viapo vyote vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo alizaliwa April 16, 1995
katika kituo cha Afya Muhimbili na kupewa cheti cha kuzaliwa namba
B.0318479 cha Julai 23, 2004.
Pia viapo hivyo vinaeleza kuwa baada ya kuzaliwa mshtakiwa, mama yake
alimpa jina la Diana Michael Kimemeta, lakini alimpeleka mtoto huyo
Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndugu zake, walimpa jina la Elizabeth, jina
la bibi yake Elizabeth Shikana.
Viapo hivyo vinaendelea kueleza kuwa baada ya majadiliano wote, yeye
mama, baba na ndugu wengine walikubaliana kuwa wamuite Diana Elizabeth
Michael Kimemeta .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment